Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, alikusudia kutoa Shilingi katika Bajeti ya Waziri Mkuu, akiitaka Serikali
na Waziri Mkuu kutoa kauli ya Kuzuia Kikosi Maalumu cha Utesaji, utekaji
udhalilishaji na mauaji kinachoratibiwa na Idara ya Usalama wa Taifa,
kwa kuwa kikundi kazi hicho kinavunja katiba na sheria za nchi.
Ushahidi wa Utekaji,udhalilishaji , Utesaji na mauaji yanayofanywa na
kikundi hicho ulitolewa na Tundu Lissu ambapo alisisima bungeni
kuelezea kuwa wapo watu 18 anaowatetea Mahakamani ambao wapo tayari
kutoa ushahidi huo, dhidi ya kikundi hicho kinachotumia nyumba iliyopo
Mikocheni na Oysterbay ambapo watu mbalimbali wamekuwa wakisafirishwa
kutoka mikoani mpaka kwenye nyumba hizo kuteswa kinyama bila jamii
kujua.Mbali na ushahidi wa wazi wa Nape kutishiwa bastola hadharani,
Bashe kutishiwa maisha na usalama wa Taifa kuwa yupo kwenye orodha ya
wabunge 11 wanaotakiwa kufanyiwa mabaya, Godbless Lema na Lissu mwenyewe
kukamatwa na polisi bila kibali cha ukamataji kuwekwa rumande na
kunyimwa dhamana, Ben Saanane kupotea, Ney wa Mitego kukamatwa, Roma
Mkatoliki kutekwa na kuteswa, Clouds Media Group kuvamiwa na mtu ambaye
Watanzania wote wanamjua na nashangaa kwanini bado ni Kiongozi wa Serikali na serikali imekaa kimya?Je,kuna baraka za Ikulu?
Jambo hilo limepingwa sana na Mawaziri wa CCM, Jenister Mhagama na
Angela Kairuki kwa kuwa wamesema hakuna habari zozote za namna hiyo,
wakidai kuwa hakuna utekaji nyara hapa nchini kuwa ni maneno ya baadhi
ya watu wa mitandaoni wanoataka kuichafua Serikali .Walimuomba Waziri
Mkuu asitoe kauli yoyote kwa kuwa jambo hilo ni uchochezi. Mawaziri hao
wameona matukio yote hayo si kitu wala si chochote katika nchi kana
kwamba walioteswa si watu wanaowahusu, wala hao hawastahili kulindwa utu
wao na kana kwamba si Watanzania. Mawaziri hao wameitetea Serikali na
kumwomba Spika kuwa Hoja hiyo isijadiliwe Bungeni.
Jambo hilo lilimpelekea Spika kutaka kura ipigwe na ndipo Wabunge walio
wengi wakaomba kujadili kwa kina na serikali itoe kauli. Spika kwa
mamlaka yake ameamua jambo hilo lisijadiliwe kabisa ndani Bunge.
Chanzo: Jamii Forum
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
0 maoni :
Chapisha Maoni