Zilizopendwa Zaidi

Wapendwa
Breaking
Inapakia...

TANZANIA INA FURSA YA KULIMA MARA 4 KWA MWAKA " HASHIM RUNGWE"

Mwenyekiti wa Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma), Hashim Rungwe amefunguka na kusema kitendo cha Tanzania kushindwa kutumia fursa ya kilimo cha umwagiliaji ni kitu ambacho kinamuumiza na kusema hicho ni kitu kinachorudisha nyuma maendeleo. [​IMG]
Mwenyekiti wa Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma), Hashim Rungwe

Rungwe amesema yeye angekuwa Rais wa nchii angehakikisha Watanzania wanalima mara nne kwa mwaka kwa kilimo cha kumwagilia na si kutegemea kilicho cha mvua, na kusema Mungu ametujalia karibu kila kitu ila tunashindwa kutumia rasimali hizo jambo ambalo linatia aibu.

"Mimi ningemwagilia kwa kutumia ndege za kumwagilia maji mabuza yale ningemwagilia mashamba. lile bonde la Shinyanga pale mimi naona aibu sana, mimi ningehakikisha Watanzania wanafanya kazi wanalima kwa mwaka mara nne siyo lazima tulime mashamba nchi nzima bali tungelima mashamba ambayo yangetupa hadhi, nasema mimi ningefanikisha" alisema Rungwe
Rungwe alikwenda mbali zaidi na kusema suala la kuhamisha maji ni jambo ambalo linawezekana na kutolea mfano nchi ambazo kiasili ni jangwa lakini saizi wanafanya kilimo baada ya nchi hizi kuchukua udongo sehemu nyingine na kupeleka kwao na kufanya kilimo.

"Kwani unafikiri huko nje wenzetu wanafanyaje, hata ukieenda hapo Israeli au ukienda Saudi Arabia nchi nzima imelimwa? Wale wanahamisha udongo kutoka nchi zenye udongo mzuri wenye rutuba wanapeleka jangwani wanatengeneza mashamba na wanapata matunda mazuri wanauza dunia nzima, sasa itakuwa sisi ambao Mungu katujalia ametupa kila kitu bure tunashindwaje kuhamisha maji, wakati Benki ya dunia ipo, IFM ipo na nchi ndiyo zamana" alisema Rungwe .

Chanzo: EATV

 
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 maoni :

Chapisha Maoni