Mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali(CAG) anawasilisha ripoti yake kwa wanahabari leo. Fuatana nami kujua atachosema.
======
Mkaguzi anasema ripoti inaonyesha fedha nyingi zaidi zilitumika katika matumizi ya kwaida kuliko matumizi ya maendeleo.
Ukusanyaji ni mdogo wa maduhuri katika kusimamia bajeti. Bila kutumia
mikopo, serikali ingeweza kugharamia asilimia 62 pekee ya bajeti yake.
Assad: Deni la Taifa limefikia trilioni 41 Juni 2016 kulinganisha
na trilioni 33 2015 na kiasi hiko hakijajumuisha trilioni nane ambalo
ni deni katika hifadhi za jamii, serikali iliadi kutoa non cash bond na
haijatimiza.
Deni la taifa linakuwa kwa kasi, zaidi ya 20% ikimaanisha baada ya miaka mitano litakuwa mara mbili. Sio vizuri deni kukua kwa namna hii.
Serikali haikuwasilisha michango kwa mifuko ya hifadhi ya jamii ya bilioni 400, si busara serikali kuchelewesha kwani hata wastaafu watacheleweshewa.
Malipo ya mishahara ya bilioni 9.8 yaliyofanyika kwa wafanyakazi waliofariki, watu wamelipwa na kodi zimekatwa, serikali ifanye juhudi kuhakikisha database yao iko updated.
Mishahara kwa kawaida isipochokuliwa benki inaitwa unclaimed salaries na inatakiwa kurejeshwa hazina lakini tumefatilia hairejeshwi na mabenki.
Pia Assad kazungumzia baadhi ya taasisi kukosa hati za malipo na kusema
anazitaka kwani sheria inamruhusu kuzidai. Magari 2172 yametelekezwa
ikiwa ni ongezeko la 88% kutoka mwaka 2015, amesema magari yaliyofikia
ukomo wa matumizi bora kuuza kama ipo busara ya kuuza au kuzipa taasisi
nyingine ambazo zinaweza kuyatumia.
Bilioni 24 imetumika bila kushindanisha tenda.
Chanzo: Jamii Forum
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
0 maoni :
Chapisha Maoni