Rais Zuma: Waandamanaji ni wabaguzi wa rangi,
Rais wa Afrika
Kusini Jacob Zuma amewataja watu wanaofanya maandamano dhidi yake kuwa
wabaguzi wa rangi akisema walibeba mabango yalioonyesha kuwadharau watu
weusi.
Maelfu ya waandamanaji walifanya maandamano baada ya kumfuta kazi waziri wake wa fedha Pravin Gordan.Maandamano hayo yalipangwa na vyama kadhaa vya upinzani na makundi kadhaa ya wanaharakati.
''Maandamno yaliofanyika wiki iliopita yalibaini kwamba ubaguzi wa rangi upo na unaendelea nchini Afrika Kusini'', alisema.
Wakati huohuo wafuasi wa rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma walivuruga hafla ya makumbusho ya aliyekuwa mwanaharakati wa kupambana na ubaguzi wa rangi, Ahmed Kathrada.
Watu hao walianza kuleta uzushi wakati aliyekuwa waziri wa fedha Pravin Gordan alipokuwa anatoa hotuba yake ambayo ilikuwa inakashifu ufisadi katika chama cha A
NC, akisema kuwa huenda chama hicho hakitashinda uchaguzi wa 2019.
Source: Swahili BBC London
0 maoni :
Chapisha Maoni