MKUU WA WILAYA YA ILALA AMEAGIZA KUBOMOA NYUMBA ZOTE MARA MOJA ZILIZOJENGWA BONDE LA MAJOHE
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema ameagiza nyumba 200 zilizopo kwenye bonde eneo la Majohe zibomolewe na waathirika wasilipwe fidia.
Hii inatokana na ujenzi wa nyumba hizo kuathiri mtiririko wa maji kwani ziko kwenye mkondo maji na husababisha maji kufurika na kuharibu miundombinu hasa barabara ya Pugu-Majohe.
Amewashangaa wananchi walionunua viwanja kwenye eneo hilo na kujenga huku wakiona ni eneo la bondeni na kuamuru ujenzi usitishwe.
Amesema kutoka kwenye bonde hadi mita 60 pande zote haitakiwi mtu kujenga na watakaojikuta wapo ndani ya umbali huo waanze kubomoa wenyewe
0 maoni :
Chapisha Maoni