Claudio Ranieri anasema alichochewa na mtu katika klabu lakini sio wachezaji,
Meneja wa zamani wa
Leicester Claudio Ranieri anaamini kuwa kuna mtu kwenye klabu aliyekuwa
anampinga lakini anasema hadhani ni wachezaji waliosababisha yeye
kupigwa kalamu.
Muitaliano huyo aliongoza klabu ya Leicester kushinda ligi kuu msimu uliopita lakini akafutwa Februari.
"Siwezi kuamini kuwa ni wachezaji wangu walionimaliza, hapana,hapana," aliwaeleza wanahabari wa spoti wa Sky "
"Labda
ni mtu mwingine tu. Nilikuwa na tatizo kidogo mwaka uliopita na
tulishinda ligi. Labda mwaka huu tutakaposhindwa, watu watatia bidii
kiasi."
Wakati Ranieri alifutwa kazi Leiceter ilikuwa pointi moja juu ya eneo la kushushwa ngazi la ligi kuu.
Meneja msaidizi Craig Shakespeare alipewa kazi yaa kuifunza timu hiyo na kuiongoza kushinda mechi tano za ligi kuu.
"Mimi husikiza mambo mengi sana," alisema Ranieri huku akikataa kusema aliyekuwa anazungumzia.
"Sitaki kusema ni nani. Mimi ni mwaminifu. Kile nilichokuwa nacho nilikisema uso kwa uso."
|
0 maoni :
Chapisha Maoni