Basi la timu ya B. Dortmund lakabiliwa na milipuko Ujerumani,
Polisi nchini
Ujerumani imesema kuwa gari lililokuwa limewabeba wachezaji wa Borussia
Dortmund kuelekea katika mchezo wa nyumbani kwenye ligi ya mabingwa
Ulaya lililengwa na milipuko mitatu.
Katika mkutano na waandishi
wa habari, wamesema kuwa barua ilikutwa pembezoni mwa eneo la shambulizi
hilo,lakini haikuwa na maelezo ya kutosha.Polisi imekana kuwa ni shambulizi la kigaidi.
Mchezaji mmoja wa Dortmund na raia wa Uhispania Marc Bartra amejeruhiwa na kufanyiwa upasuaji.
Taarifa za kiintelijensia zinasema kuwa zinachunguza shambulizi hilo kama linahusika na mashabiki wa timu ya upinzani.
Mchezo kati ya Dortmund na Monaco umeahirishwa mpaka Jumatano.
Source: BBC SWAHILI
0 maoni :
Chapisha Maoni