Zilizopendwa Zaidi

Wapendwa
Breaking
Inapakia...

BIASHARA YA UTUMWA YAKAMATA KASI WAAFRIKA WANAUZWA LIBYA

Waafrika wanauzwa Libya katika biashara ya utumwa

Ripoti ya IOM yasema kuwa wahamiaji wa kiafrika wananunuliwa na kuuzwa katika Libya 

Ripoti ya IOM yasema kuwa wahamiaji wa kiafrika wananunuliwa na kuuzwa katika Libya

Raia wa Afrika wanaojaribu kuvuka na kuelekea barani Ulaya, wanauzwa na watekaji wao na kuuzwa katika "soko la utumwa" nchini Libya. Hayo yamesemwa na shirika la kuwahudumia wahamiaji duniani International Organization for Migration (IOM).
Wahasiriwa wameiambia IOM kuwa, baada ya kuzuiliwa na walanguzi wa biashara ya watu au makundi ya wapiganaji, wanapelekwa hadi kwenye viwanja vya mji au kwenye maeneo ya kuegeshea magari na kuuzwa

Wahamiaji walio na ujuzi kama vile upakaji rangi au ukulima, wanauzwa kwa bei ya juu, kiongozi mkuu wa shirika hilo la IOM nchini Libya ameiambia BBC
Libya imekuwa katika ghasia tangu mwaka 2011 pale wanajeshi wa shirika la kujihami la mataifa ya magharibi-NATO yalipomuondoa madarakani Rais wa nchi hiyo Kanali Muammar Gaddafi.

IOM yasema matendo ya

 OM yasema matendo ya "kutisha" dhidi ya wahamiaji inajumuisha kula chakula kidogo, kuuwawa au kuachwa wafe njaa

Kwa mjibu wa IOM, maelfu ya wanaume chipukizi kutoka mataifa ya kusini mwa jangwa la Sahara wameuzwa katika masoko hayo ya utumwa wa binadamu.
Mhamiaji mmoja kutoka Senegal, ambaye jina lake limebanwa ili kumlinda, amesema kuwa amewahi kuuzwa katika masoko kama hayo katika mji wa Sabha kusini mwa Libya, kabla ya kuwekwa katika gereza moja bovu, ambapo zaidi ya wahamiaji 100 walikuwa wakizuiwa.
Kila mwaka maelfu ya wahamiaji huvuka bahari ya Mediterranean kuelekea Bara Ulaya
Kila mwaka maelfu ya wahamiaji huvuka bahari ya Mediterranean kuelekea Bara Ulaya
Amesema kwamba, wahamiaji wanaozuiliwa waliambiwa kuwapigia simu familia zao, ambao waliulizwa kutoa fedha ya kikombozi ili waachiwe huru, na baadhi yao wakapigwa wakiwa bado wanazungumza kwenye simu, ili kuwafanya jamaa zao wasikie wakiteswa ili watume haraka fedha hizo.
Ameelezea kuwa ni matendo ya "kutisha" ambapo wahamiaji walilazimishwa kuhimili kula kiwango kidogo mno cha chakula, lakini kwa wale wasioweza kulipia wanauwawa au wanaachwa ili wafe njaa, ripoti hiyo inaongeza.

Source: Swahili BBC



 

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 maoni :

Chapisha Maoni