Wakazi wa Kata ya Mwaya Tarafa ya Mang'ula Wilayani Kilombero mapema leo wamejitokeza kwa wingu kumpokea Mbunge wa Jimbo la Kilombero Mhe Peter Lijualikali katika Mkutano wake na wakazi wa Kata hiyo.
Lijualikali aliwataka wakazi hao kutokuwa na uwoga na badala yake waunganishe nguvu zao kwa kushirikiana na viongozi waliowachagua licha ya viongozi hao kufanyia vikwazo vingi.
Akiwashukuru wakazi hao juu ya upendo waliouonyesha dhidi yake tangu alipofungwa Lijualikali aliwaahidi kufanya kazi waliyomtuma kwani kifungo chake kimetokana na chuki za kisiasa juu ya kupigania haki ya wananchi wa Jimbo lake.
Maendeleo
Lijualikali alilaani kitendo cha Magereza kumnyika kuweka saini Mkataba wa mradi wa ujenzi wa daraja la DDC ambalo linaunganisha Kata ya Mangula na Kata ya Mwaya hali ambayo imewafanya wakazi wa kata hizo kukosa huduma kutoka kwa Mbunge wao.
Akizungumzia ujenzi wa barabara kutoka kidatu mpaka ifaka Lijualikali alisema "Taratibu zote za msingi zimeshafanyika hatua ya inayofata ni wafadhi wa ujenzi huo wanafanya tathmini na ujenzi utaanza mwishoni mwa mwezi wa tano.
Hali ya Kisiasa
Akizungumza na wakazi hao Lijualikali alizungumzia hali ya Kisiasa nchini ambapo amewaeleza hakuna aliyesalama na endepo wenye kuweza kupiga kelele basi wapige kelele kulaani vitendo vya Serikali kuwakandamiza viongozi wa upinzani.
Lijualikali amemaluza ziara yale ya siku mbili Jimboni kwake ikiwa ni mara yake ya kwanza tangu atoke Gerezani
About Unknown
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 maoni :
Chapisha Maoni