Zilizopendwa Zaidi

Wapendwa
Breaking
Inapakia...

KAULI YA NAPE, "NIMETOA CCM ILIKUWA SHIMONI" YALETA TAFRANI

Kufuatia kauli ya Mhe Nape kwamba ccm aliikuta shimoni wakati wengine walikuwa wanakunywa, KIU wa CCM ameitolea ufafanuzi,

[​IMG]
Katibu wa Itikadi na Uenezi (KIU) wa CCM, Humphrey Polepole akizungumza na waandishi wa Mwananchi Communications Limited (MCL) wakati alipotembelea chumba cha habari cha kampuni hiyo, Tabata Relini jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Katibu wa UVCCM wa Makao Makuu Idara ya Vyuo Vikuu, Debora Charles. Picha na Salim Shao

  • Nape, ambaye alikuwa akishikilia nafasi ya Polepole kabla ya Uchaguzi Mkuu, alisema maneno hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari Machi 23, siku moja baada ya kuachwa katika mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri.
  • Nape aliyetishiwa bastola kabla ya mkutano huo, alikuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Dar es Salaam. Katibu wa Itikadi na uenezi wa CCM, Humphrey Polepole amekitaka chama hicho kumwajibisha Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye kwa kauli yake kuwa alikitoa chama hicho shimoni.

Nape, ambaye alikuwa akishikilia nafasi ya Polepole kabla ya Uchaguzi Mkuu, alisema maneno hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari Machi 23, siku moja baada ya kuachwa katika mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri.

Nape aliyetishiwa bastola kabla ya mkutano huo, alikuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

“Wamesahau wakati mimi nalala porini, wenyewe walikuwa wanakunywa bia baa. Nimekuwa mzalendo kwa nchi yangu, nimekuwa muungwana kwa chama changu na ninaapa kuwa muungwana kwa nchi yangu, hilo hakuna atakayelibadilisha. Lakini mimi nimekuwa mzalendo kwa CCM ambayo nimeikuta kwenye shimo inakwenda,” alisema Nape.

Lakini Polepole, ambaye jana alitembelea ofisi za kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL) inayozalisha magazeti ya Mwananchi, The Citizen na Mwanaspoti, alisema kama Nape alitoa kauli hiyo, alikuwa amekengeuka.

“Amekitoa Chama cha Mapinduzi shimoni? Kwamba, wakati anakitoa chama shimoni wengine walikuwa wanafanya nini?” alihoji Polepole.
 
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 maoni :

Chapisha Maoni