Zilizopendwa Zaidi

Wapendwa
Breaking
Inapakia...

GHANA YAUWA UCHUMI WA KODI YAPANDISHA WA UZALISHAJI

Rais Mpya wa Ghana Nana Akufo-Addo, miaka 73, wa chama cha NPP aliyeingia madarakani tarehe 7 mwezi Januari 2017 amefanya mapinduzi makubwa ya kifikra na kimfumo kuwahi kutokea barani Afrika katika miongo ya karibuni. Amekusudia kufanya mambo mawili makubwa, kwanza kujenga uchumi rafiki kibishara na pili kujenga mazingira rafiki na bora kwa kila mtu kuliko nchi yoyote ya Afrika. Na ameonyesha kwa vitendo nia na uwezo wake wa kutekeleza hayo maono mawili:- 1) Ameondoa kodi ya Thamani VAT kwenye mauzo ya real estates! 2) Ameondoa kodi ya Thamani VAT kwenye huduma za kifedha! 3) Ameondoa kodi ya Thamani VAT kwenye mauzo ya hisa kwenye soko la hisa! 4) Ameondoa ushuru (import duty) kwenye vipuri (spare parts)! 5) Ameondoa asilimia 1% ya tozo (import levy)! 6) Ameondoa kodi ya VAT kwenye tiketi za ndege kwa safari za ndani! 7) Amepunguza kwa kiwango kikubwa kodi ya VAT kwa wafanyabiashara wadogo kutoka 17.5% mpaka asimilia 3% tu! 8) Wanaendelea na majadiliano ya kikanda kwenye jumuiya ya ECOWAS ili kuondoa kabisa ushuru (import duties) kwenye malighafi na mashine zitakazoingizwa Ghana. Mwenyezi amsaidie na kumbariki sana Rais Nana na wananchi wa Ghana. Hii inathibitsha kuwa pasipo na maono watu wanaangamia, lakini penye maono na kiongozi mwenye fikra, uwezo na umoja tena kwa kufuata mfumo wa kidemokrasia (sio kwa shuruti na ukali) nchi na jamii husika vinaweza kupiga hatua kubwa sana. Ni matukio machache kama hili yanayonifanya kuona fahari kuwa Mwafrika. Mabadiliko na namna ambayo Rais Nana na Serikali yake wanavyofanya, ni ya kujivunia kwa kila Mwafrika na mpenda maendeleo duniani.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 maoni :

Chapisha Maoni