Zilizopendwa Zaidi

Wapendwa
Breaking
Inapakia...

WAJUE MABINTI WA MARAIS WENYE MAMLAKA NA USHAWISHI MKUBWA DUNIANI

Binti kama baba: Mabinti wa marais wenye mamlaka na ushawishi duniani

Ivanka Trump kando ya baba yake , Donald Trump
Ivanka Trump tayari ni mfanyabiashara na mtu binafsi maarufu

Akiwa na ofisi yake binafsi katika ikulu ya White house, Ivanka Trump ni mwanamke ambaye hadhi yake imeimarika kama mmojawapo wa wanawake wenye mamlaka makubwa katika utawala wa Donald Trump.

Ivanka mwenye umri wa miaka 35 atahudumu kama ''macho na masikio'' ya Donald Trump, lakini hatakuwa na cheo rasmi wala mshahara atakapokuwa akifanyia kazi katika jengo la West Wing ambalo ni sehemu ya White House.
Mwanamke huyo aliyefanikiwa kibiashara na ambaye ni mtu maarufu ni mwanamke wa hivi karibuni kujumuishwa katika orodha inayoongezeka ya mabinti wa hadhi ya juu ya wakuu wa nchi kote duniani.
Mwandishi wa BBC Valeria Perasso anaangazia majukumu tofauti ya baadhi ya mabinti wa marais wenye ushawishi.

 Mabinti wa marais wa Urusi , Tajikistan, Pakistan, Angola, Cuba na Uturuki ( Kutoka juu kushoto)

Maryam Nawaz Sharif akisalimia umati wa watu
Maryam Nawaz Sharif alikuwa na jukumu kubwa katika kampeni za kuchaguliwa tena kwa kwa baba yake

Kampeni ya familia,

Maryam Nawaz Sharif, mwenye umri wa miaka 43, ni binti yake Waziri Mkuu wa Pakistani Nawaz Sharif.
Mwanzo alijihusisha na shughuli za shirika la familia la misaada, baadaye Bi Nawaz alitekeleza jukumu kubwa la kuwa meneja wa kampeni za uchaguzi katika mwaka 2003 zilizofanikisha kuchaguliwa tena kwa baba yake.
Kwa sasa anahudumu katika chama cha baba yake cha mrengo wa kulia kinachofahamika kama - Pakistan Muslim League (Nawaz).
"Amekuwa mtu wa kuangaziwa mara kwa mara," anasema mwandishi wa BBC idhaa ya Urdu Asif Farooqi, ambaye amekutana naye mara kadhaa.
"Kusema ukweli amejitokeza kama mtu mwenye mamlaka makubwa, na kama mtu atakayemrithi baba yake."
Mwaka jana jina lake lilijitokeza katika kile kilichofahamika kama - nyaraka za Panama, ambapo taarifa zilidai yeye na kaka zake wana uhusiano na sakata ya umiliki wa mali zisizofahamika katika mataifa ya kigeni na akaunti zinazotumiwa kununua mali za kifahari jijini London.
Baba yake alipuuzilia mbali shutuma hizo akitaja taarifa hizo ambazo alisema ni kazi ya watu "wanaonilenga pamoja na familia yangu kwa malengo ya kisiasa".
Shutuma hizo zinachunguzwa na Mahakama ya Juu ya Pakistan na uamuzi unatarajiwa kutangazwa wiki kadhaa zijazo .
Katerina Tikhonova akidensi na Ivan Klimov wakati wa mashindano ya dunia ya Rock'n'Roll Acrobatic mjini Krakow, 2014
Binti yake tais Vradimir Putin wa Urusi Yekaterina ni mchezaji maaruru wa mashindano ya densi ya rock and roll   

Densi ya Rock and Roll
Rais wa Urusi Vladimir Putin anafahamika kwa kulinda maisha yake ya kibinafsi, na ni hivi karibuni tu ambapo taarifa chache tu zilijulikana kuhusu maisha ya mabinti zake wawili.
"Maafisa wa Urusi huangalia nia yoyote ya vyombo vya habari kama jambo la kushukiwa," anasema mwandishi wa BBC wa Urusi Famil Ismailov.
"NI jukumu la waandishi wa habari wenyewe kujaribu ni wapi wanaweza kufikia kupata habari na taarifa nyingi hazijawahi kuthibitishwa na familia."
Mwaka 2015, binti mdogo wa rais Putin, Yekaterina, allijitokeza hadharani baada ya kufichuliwa kwa taarifa kuwa alikuwa akiishi mjini Moscow akitumia jina la Katerina Tikhonova.

 Source:BBC LONDON

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 maoni :

Chapisha Maoni