Samsung kupoteza faida ya £4.4bn kutokana na Note 7
Kampuni ya Samsung imesema gharama
ya kuacha kuuza simu yake ya karibuni zaidi ya Galaxy Note 7 sitakuwa
zaidi ya £4.4bn ($5.4bn).
Kampuni hiyo ya Korea Kusini tayari imepunguza matarajio yake ya faida ya robo ya tatu ya mwaka kwa £1.9bn ($2.3bn). Mnamo Ijumaa, kampuni hiyo ilisema inatarajia kuathirika zaidi na kupoteza won 3.5 trilioni zaidi ($3bn, £2.5bn).
- Samsung: Zimeni simu za Note 7 ni hatari
- Kwa nini betri za Lithium hulipuka?
- Samsung yasema haitaunda tena Galaxy Note 7
Hitilafu ilidhaniwa kuwa kwenye betri.
Kampuni hiyo hata hivyo iliacha kuunda na kutengeneza simu hizo baada ya simu mpya walizokuwa wamebadilishiwa wateja, ambazo zilidhaniwa kuwa salama, kuanza kushika moto.
Simu hiyo ilikuwa imezinduliwa Agosti ikitarajiwa kushindana na simu mpya ya Apple iPhone7.
Licha ya matatizo hayo, Samsung Electronics imesema inatarajia kupata faida ya won 5.2 trilioni (£3.7bn) robo ya tatu ya mwaka huu.
0 maoni :
Chapisha Maoni