Mikebe ya Coca Cola yagunduliwa kuwa nakinyesi cha binadamu
Coca Cola |
Polisi wameanzisha uchunguzi wa kile
kilichoonekana kuwa kinyesi cha binadamnu, kupatikana kwenye mikebe ya
kujazwa soda iliyowasilishwa kwa kiwanda cha Coca Cola huko Ireland
kaskazini.
Shughuli za usiku katika kiwanda cha Lisburn zilivurugwa wiki iliyopita wakati mashinde zilikwama.Coca-Cola ina kiwanda kikubwa huko Lisburn |
Kampuni hiyo ilisema kuwa kisa hicho hakikuathiri vinywaji vyovyote ambavyo kwa sasa viko sokoni.
Polisi wanachunguza ripoti kuwa mikebe mingi huenda ilichafuka.
Kiwanda cha Coca Cola cha Knockmore, Lisburn |
Msemaji wa Coca-Cola amesema kuwa kampuni hiyo ilikuwa ikifahamu kisa hicho cha mikebe mitupu katika kiwanda cha Knockmore.
"Tatizo hilo lilitambuliwa mara moja na bidhaa zote zilizoathirika kuzuiwa na haziwezi kuuzwa. Hiki ni kisa kilicho kando na hakiathiri biddaa zozote zilizo sokoni."msemaji wa Coca Coa alisema.
0 maoni :
Chapisha Maoni