Zilizopendwa Zaidi

Wapendwa
Breaking
Inapakia...

GWAJIMA ATEMBELEA OFISI ZA CLOUDS MEDIA

Mchungaji wa kanisa la ufufuo na uzima, Josephat Gwajima amewasili ofisi za clouds media kama alivyoahidi. 


Kiongozi huyo wa kanisa la ufufuo na uzima amefika katika ofisi hizo saa 4:00 asubuhi akiwa na msafara wa magari zaidi ya manne huku yeye akiwa kwenye gari aina ya Hammer na kupokelewa na mwenyeji wake Ruge Mutahaba. Gwajima amesema ameenda Clouds kwa sababu yeye ni sehemu ya stori na hio sio stori ya kisiasa. Amedai clouds wamefanya huo ufafanuzi kwa nia njema, kutaka kuombwa radhi na mtu mmoja alietumia madaraka yake vibaya na sio serikali.

Akiwa hapo Askofu Gwajima pia alipata fursa ya kujibu maswali mbalimbali ya waandishi wa habari waliokuwepo katika ofisi hizo.

Swali(Mtanzania): Kwanini unafikiri wewe ni chanzo?

Jibu(Gwajima): Jina langu lilikuwa miongini mwa yaliyotajwa na nikiwa kiongozi wa dini pekee. Sijawahi kutumia kilevi cha aina yeyeto, walifanya uchunguzi wa madawa na money laundering hawakunikuta na hatia. Nilipofatilia inawezekanaje mtu akataja watu bila ushahidi nikagundua ndugu yetu hakumaliza elimu.

Watu wengi wamepoteza nafasi zao kwa ajili ya vyeti ikiwemo wanafunzi na wafanyakazi, inakuwaje mtu mmoja yeye ameachwa.

Swali(Global): Inasemekana wewe na mkuu wa mkoa mna interest ya jimbo moja

Jibu: Naita ni kuogopa tembo ambae hajazaliwa, Kolomije ambayo ipo jimbo la Misungwi ni nyumbani kwetu na sina nia ya nia ya jimbo, kuogopa kitu ambacho hakipo hakina maana sana kwa ambae amesoma, inayeogopa una-question shule yake. Nina watoto watatu, sina mtoto mwingine na hata angekuwepo ningelea lakini siwezi kulea mtoto ambae sio wangu.


Source; jamii forum

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 maoni :

Chapisha Maoni