KESI YA KITILYA: Korti Kisutu, Dar yafuta shtaka la kutakatisha fedha dhidi ya aliyekuwa bosi wa TRA, Harry Kitilya, wengine 2. Mawakili sasa wanaomba dhamana.
================
Kamishna Mkuu Mstaafu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Harry Kitilya (kushoto) akiwa na waliokuwa Wafanyakazi wa Benki ya StanBic Tanzania, Sioi Sumari (katikati) na Shose Sinare, wakiwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Jijini Dar es salaam.
Washitakiwa hao wanaokabiriwa na mashtaka nane likiwemo la utakatishaji Fedha kiasi cha Dola za Marekani milioni 6, ili kufanikisha mkopo kutoka Benki ya Stanbic kwenda Serikalini, walifikishwa Mahakamani hapo leo kusikiliza keshi yao, na walifanikiwa kufutiwa Shitaka moja la kutakatisha Fedha kati ya nane yaliyokuwa yakiwakabili, ambapo Washitakiwa hao walisomewa kufutwa kwa shitaka hilo kwa madai ya kukosa Vidhibitisho.
Baada ya kufutiwa shitaka hilo, DPP aliwasilisha hati ya mapendekezo ya kukata rufaa ya kupinga uamuzi wa kufuta shitaka namba nane la utakatishaji Fedha linalowakabili watuhumiwa hao, ambapo zoezi la dhamana liligonga mwamba na Washitakiwa hao wamerudishwa rumande mpaka April 29 2016 ambapo mahakama itatoa maamuzi kama watuhumiwa watapewa dhamana.
Chanzo: Michuzi
About Unknown
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 maoni :
Chapisha Maoni