Zilizopendwa Zaidi

Wapendwa
Breaking
Inapakia...

VIDEO YA NDESAMBURO ENZI YA UHAI WAKE

May 31, 2017 kiliripotiwa kifo cha Mbunge wa zamani wa Moshi Mjini na Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Kilimanjaro Philemon Ndesamburo na kuthibitishwa na Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe.
Leo June 1, 2017 Viongozi wa CHADEMA wakiongozwa na Katibu Mkuu Vincent Mashinji na mmoja wa waasisi wa chama hicho Victor Kimesera wamekutana na Waandishi wa Habari kueleza mambo kadhaa yaliyofanywa na Ndesamburo.
Victor Kimesera ameeleza baadhi ya mambo hayo yaliyofanywa na mzee Ndesamburo kwenye chama hicho, ikiwa ni pamoja na kusaidia ununuzi wa Jengo la Ofisi ya Makao Makuu kwa Tsh. 12m pamoja na kusaidia kupatikana magari mawili yaliyosaidia kuzunguka sehemu tofauti kupata wanachama.
Kwenye VIDEO hii hapa chini kuna mambo yote ambayo ameyafanya mzee Ndesamburo kwa CHADEMA enzi za uhai wake…unaweza kutazama kwa kuonyeza play hapa chini kutazama!!!

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 maoni :

Chapisha Maoni