Zilizopendwa Zaidi

Wapendwa
Breaking
Inapakia...

NECTA WALAAMIKIWA KUACHA SHUGHULI ZA KAWAIDA KWA KUWASHUGHULIKIA WALIOKUMBWA NA VYETI FEKI

Image result for picha katibu mkuu baraza la mitihani
KATIBU MKUU NECTA
Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) limeamua kusimamisha shughuli nyingine zote barazani hapo ili kushughulikia rufaa za watumishi waliotangazwa na serikali kwamba walifoji vyeti.
Leo katika viunga vya baraza hilo nimeshuhudia umati mkubwa wa watumishi, wengi kutoka mikoani wakiwa wamefurika hapo wengi wakilalamika waliingizwa kwenye orodha ya wenye vyeti feki kimakosa.

Kutokana na Necta kuelemewa na idadi kubwa ya wakata rufaa hao, uongozi ukatangaxia wananchi wengine waliofika kwa shughuli nyingine kwamba kwa sasa hakuna mtu mwingine yeyote atakayehudumiwa zaidi ya hao watumishi wenye malalamiko ya kuingizwa kimakosa katika orodha ya wenye vyeti vyeki!
Hata hivyo wateja wengine wa Baraza la Mitihani wamelaumu uongozo wa Baraza kwa uamuzi huo. Wamedai kwamba nao pia wanahaki ya kuhudumiwa. Na pia wameshangazwa na bodi kusimamisha huduma nyingine badala ya kujipanga kuwahudumia wateja wao wote kwa utaratibu maalum badala ya kuahirisha huduma kwa muda usiojulikana!

Source:Jamii Forum
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 maoni :

Chapisha Maoni