Zilizopendwa Zaidi

Wapendwa
Breaking
Inapakia...

ALBERT MSANDO AJIUZULU NAFASI YAKE YA USHAURI ACT, ZITTO AMKUBALIA

Image result for albert msando na zitto kabwe images
                     KUSHOTO WAKILI A. MSANDO, KULIA MHE ZITTO KABWE

Kwa Kiongozi Mkuu wa Chama,
YAH: KUJIUZULU NAFASI YANGU YA MSHAURI MKUU WA CHAMA.
Napenda kuchukua nafasi hii kukujulisha uamuzi wangu wa kujiuzulu nafasi yangu kama Mshauri Mkuu wa Chama. Uamuzi huu ni kutimiza hitaji langu la kuishi kama mfano kwa jamii inayonizunguka. Kama kiongozi nastahili kuwajibika kutokana na video clip iliyorekodiwa na kusambazwa. Ni wajibu wangu kwa chama changu na nchi yangu kuwajibika kama kiongozi.

Nitaendelea kuwa mwanachama mtiifu nikishirikiana nawe kujenga chama na kuhakikisha nchi yetu inaendelea mbele. Nakushukuru kwa kuniamini kwa kipindi chote tulichofanya kazi pamoja.
Wako
Albert G. Msando #TheDon

-----------
Nimepokea barua ya Wakili Albert G. Msando kuomba kujiuzulu nafasi yake ya Ushauri wa Chama chetu cha ACT Wazalendo.

Ndugu Msando anawajibika Kwani anapaswa, nanukuu "kuishi Kama mfano Kwa jamii inayonizunguka".

Ndugu Albert Msando amekuwa kiongozi mwenye mchango mkubwa katika chama katika nafasi mbalimbali alizoshika ndani ya chama. Chama kinamshukuru kwa moyo wake wa kuzalendo na mchango alioutoa katika Chama. Ni matumaini yetu ataendelea kushirikiana nasi katika ujenzi wa chama kwa kadri atakavyoweza na atakapohitajika kama mwanachama.

Nikiwa Kiongozi wa Chama nimekubali kuwajibika kwake na kumtakia kheri katika kujisahihisha kwake.

Ndugu Msando Alberto ameomba msamaha Kwa jamii kwa uwazi na ni wajibu wetu kumsaidia kupita katika mitihani iliyomkumba.

Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 maoni :

Chapisha Maoni