Zilizopendwa Zaidi

Wapendwa
Breaking
Inapakia...

JENGO LA YANGA KUPIGWA MNADA WAKATI WOWOTE KUTOKANA NA DENI LA MIL 300


[​IMG]Jengo la Makao Makuu ya Klabu ya Yanga lililoko makutano ya mtaa wa Jangwani na Twiga Kariakoo jijini Dar es salaam, liko hatarini kupigwa mnada kutokana na deni la Sh. milioni 300 ambazo klabu hiyo inadaiwa, imefahamika.

Taarifa zilizopatikana jana jijini zinaeleza kuwa kampuni ya udalali ya Msolopa ndiyo imepewa mamlaka ya kusimamia mnada huo.

Akizungumza na gazeti hili jana jioni, Katibu Mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa, alithibitisha kuwepo kwa deni hilo na kueleza kuwa uongozi umeanza utaratibu wa kulifanyia kazi suala hilo.

Mkwasa alisema kuwa deni hilo limetokana na malimbikizo ya ada ya jengo la kiwanja kinachomilikiwa na klabu hiyo, lakini wanaamini watalilipa kabla ya mchakato huo wa kunadi jengo hilo la Makao Makuu haujafanyika.

"Ni kweli kesi iko katika mahakama ya Ardhi na tumeshaanza kuifanyia kazi", alisema kwa kifupi Mkwasa, Kocha na Mchezaji wa zamani wa timu hiyo.

Chanzo: Nipashe
 
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 maoni :

Chapisha Maoni