Hata baada ya Azimio la Zanzibar la kuweka ccm kwenye ubepari , Marehemu Sozigwa aliendelea kuishi kijamaa hadi mauti ilipomkuta, aliamini katika undugu, usawa, haki na heshima kwa kila binadamu kama nguzo kuu ya maisha ya mwanadamu awapo hapa duniani
Kwa maoni yangu, sifa kuu inayompambanua mzee Sozigwa katika maisha yake yote ya siasa hapa alihubiri kile alichokiamini.
Katika miaka ya sabini, akiwa mkugenzi wa Redio Tanzania, alianzisha
kipindi redioni kilichojulikana kwa jina la; "Mikingamo" katika mojawapo
ya vipindi vyake, alisema kuwa ubepali ulikuwa unyama. Na kweli, mzee
Sozigwa hata baada ya kusambaratika kwa siasa ya ujamaa aliendelea
kuishi kama mjamaa.
Nakumbuka mwishoni mwa miaka ya 1990, akiwa mjumbe wa halmashauri kuu ya
CCM alikuja Bukoba kwa shughuli za kikazi; mh. Kimiti wakati huo akiwa
mkuu wa mkoa (k) alimtumia gari ya kwenda kumpokea melini; dereva
alipomtafuta katika vyumba vyote vya daraja la kwanza hasimpate akarudi
na kuripoti kwa bosi wake kuwa mzee hakuja; kumbe yeye alikuwa amekuja kwenye daraja ya tatu. Baadaye alimpigia mh. Kimiti kumjulisha kuwa alikuwa tayari amewasili na amefikia coffee Tree Inn.
Baadaye wakati tukinywa chai pamoja yule dereva alikuja kuomba msamaha huku akijitetea kuwa alikuwa amepita kwenye vyumba vyote vya daraja la kwanza lakini hakumuona.
Kitu alichomjibu mzee yule ni;"wewe nani alikwambia kuwa chama kina fedha za kupoteza kwa kusafirisha watu daraja la kwanza." Na aliyasema hayo miaka mingi baada ya azimio la Zanzibar kuiweka CCM katika njia ya ubepari.
Wakati wa mchakato wa kumpata mgombea wa urais kupitia CCM wakati wa
uchaguzi mkuu wa 2005, sekretariati ya CCM chini ya Philip Mangula
iliazimia kuondoa mgombea yeyote atakakayebainika kutoa rushwa kwenye
kinyanganyiro.
Mzee Sozingwa akiwa anasimamia idara ya nidhamu katika sekretariati hiyo
akalivalia njuga azimio hilo, Nakumbuka wakati Kikwete alipokuja Bukoba
kusaka wadhamini, mzee Sozigwa alikuwepo akifuatilia nyendo zote
zilizoashiria kuwepo kwa mazingira ya rushwa.
Inasemekana wakati wa kujadili wagombea urais katika kamati kuu taarifa
aliyokuwa ameiandaa ilitupwa kapuni, na hatimaye sekretarati yote
ilifungiwa virago baada ya JK kuukwea wenyekiti wa CCM.
Home
/
Uncategories
/
AKIWA MKUU WA NIDHAMU, ALIFUATILIA NYENDO ZA JAKAYA UCHAGUZI 2005, TAARIFA YAKE IKAWEKWA KAPUNI,BAADA YA KUUKWA UENYEKITI WA CCM TAIFA
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
0 maoni :
Chapisha Maoni