Zilizopendwa Zaidi

Wapendwa
Breaking
Inapakia...

ZITTO AKIRI KUPOKEA BARUA YA KITILA MKUMBO YA KUJIUZULU NAFASI YA USHAURI WA CHAMA

Zitto anasema walifanya mashauriano kama chama ikiwemo Kitila Mkumbo, chama kimepokea uteuzi wa Kitila kuwa katibu mkuu. Uteuzi unaonyesha upinzani kuna watu wenye uwezo, weledi na uzalendo wa kuweza kutumika katika utumishi wa Umma.


Zitto: Kitila ni mtumishi wa umma kwa sababu ni mhadhiri wa chuo kikuu cha Dar es Salaam kwa hio nafasi aliyopata ni kupanda cheo tu ndani ya utumishi wa umma, ni sawa kama angeteuliwa kuwa Vice Chancellor wa chuo kikuu.

Kwa nafasi ya katibu mkuu, Ndugu Kitila hawezi kuendelea kuwa mshauri wa chama, nafasi ambayo inamfanya ahudhurie vikao vyote vya chama kuanzia ngazi ya chini mpaka kamati kuu na kamati ya uongozi.

Prof. Kitila ameandika barua ya kujiuzulu ushauri wa chama, nimeipokea barua yake na nimemkubalia kujiuzulu kwake kuanzia Leo. Chama kinamshukuru sana mheshimiwa Kitila kwa wakati wote alichokitumikia chama toka tulipoanza chama hiki alipokuwa mshauri wa chama.

Kaulimbiu yote siku zote ni taifa kwanza, leo na kesho hivyo tunamtakia kila laheri ndugu Kitila katika nafasi hii mpya, wizara ni kubwa na muhimu katika nchi yetu.

Zitto amesema hawawezi kuwanyima watanzania mtu mwenye weledi kwa kuweka maslahi ya chama mbele, amedai Kitila hawezi kukataa uteuzi kwa sababu yuko kwenye utumishi wa umma na hiyo ni nafasi tu kama ya kupanda cheo.

Zitto amesema hio inaonyesha kuna watu nje ya chama cha mapinduzi wanaoweza licha ya Rais Magufuli kujua anatoka upinzani.
 
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 maoni :

Chapisha Maoni