DR SERGIO CANAVERO MPANDIKIZAJI VICHWA |
Kwa mujibu wa Daktari atakayeongoza upasuaji huo Dr. Sergio Canavero, upasuaji huo utafanyika kwa mara ya kwanza kwa binadamu ambapo kichwa cha binadamu aliye hai kitapandikizwa kwenye mwili wa mtu aliyekufa na binadamu huyo kuweza kupata mwili mpya.
Madhumuni ya upasuaji huu ni kusaidia watu waliopata magonjwa ya kupooza viungo, watu wenye vilema vya miguu na magonjwa ya uti wa mgongo kupata matumaini mapya ya kuwekewa mwili mwingine. Upasuaji huu unatajwa kugharimu zaidi ya Dollar millioni 30.
Upasuaji utafanywa kwa mara ya kwanza kwa mgonjwa Valery Spiridonov kutoka
Urusi ambaye kitaondolewa kichwa chake na kupandikizwa kwenye mwili wa mtu aliyekufa. Valery Spiridonov amejitolea kufanyiwa upasuaji huou kwa sababu ana tatizo la uti wa mgongo liliopelekea mwili wake kupata ugonjwa wa kiharusi.
0 maoni :
Chapisha Maoni