Mwanaharakati akamatwa kwa 'kumtusi' Janet Museveni,
Maafisa wa polisi
nchini Uganda wamemkatama msomi mmoja ambaye amekuwa mkosoaji mkubwa wa
familia ya rais Museveni katika taifa hilo la Afrika Mshariki.
Stella
Nyanzi ,mtafiti katika chuo kikuu cha Makerere alikamatwa siku ya
Ijumaa kwa kukiuka sheria dhidi ya utumizi mbaya wa kompyuta ,kulingana
na msemaji wa polisi Asan Kasingye.Nyanzi atashtakiwa siku ya Jumatatu kwa makosa hayo kwa kutumia tarakalishi kunyanyasa mbali na kuandika maneno ya kukera.
Nyanzi ni maarufu katika mtandao wa facebook kwa ukosoaji wa rais Yoweri Museveni ambaye ameliongoza taifa hilo tangu 1986.
Wakosoaji wa Museveni wanaonya kuwa rais huyo anataka kuliongoza taifa hilo kwa maisha.
Baadhi ya mawakili wa Uganda wamekuwa wakisema wataunga mkono pendekezo la kuondoa kiwango cha umri katika katiba hatua ambayo huenda ikawa ya mwisho ya uongoza wa maisha wa rais Museveni.
Katika ukurasa wake wa facebook Nyanzi alimkemea mke wa rais, Janet Museveni ambaye ni waziri wa elimu kwa kusema serikali haina fedha za kununua sodo kwa wasichana masikini wa shule licha ya rais aliahidi kuwahifadhia fedha wakati alipkuwa akifanya kampeni za uchaguzi mwaka uliopita.
Wasichana wengi nchini Uganda wameripotiwa kuacha masomo kutokana na aibu ya kukosa sodo.
''Ninakataa wazo kwamba mtu hawezi na hafai kukosoa watu wanaonyanyasa haki na mali za Waganda katika miaka 31 ya uongozi wa kidikteta wa familia moja'', alisema katika chapisho moja la facebook.
''Kama mtu anayefikiri, msomi, mshairi, mwandishi mmiliki wa akaunti ya facebook na mtayarishaji ni jukumu langu kuwakosoa wafisadi wa siku hizi''.
Lakini mashabiki wake wanasema yeye ni mwanaharakati mwaaminifu ambaye hutumia ujuzi wake wa fasihi kupigania maskini.
Source: BBC Swahili
0 maoni :
Chapisha Maoni