Watanzania kufanya miamala ya kifedha kupitia Halopesa na NMB
Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya simu ya Halotel Le
Van Dai akibadilishana hati za makubaliano na Kaimu Mkuu wa Akiba za
Watu Binafsi wa Benki ya NMB, Boma Raballa ambapo wateja wa Halotel
watafaidika na huduma za kifedha za Halopesa kwa ataweza kuchukua na
kuweka fedha zake kutoka katika akaunti yake ya NMB. Makubaliano hayo
yalifanyika jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Ofisa Mwendeshaji wa
Halopesa, Henry Mavula na kulia ni Meneja wa Huduma za Ziada wa benki ya
NMB,Stephen Adili.
KATIKA kufanikisha azma ya kupanua wigo wa huduma za kifedha kwa wananchi wenye vipato tofauti, kampuni ya mawasiliano ya Halotel na benki ya NMB zimeingia katika ushirikiano utakao wawezesha mamilioni ya watanzania kunufaika na huduma za kifedha nchi nzima.
KATIKA kufanikisha azma ya kupanua wigo wa huduma za kifedha kwa wananchi wenye vipato tofauti, kampuni ya mawasiliano ya Halotel na benki ya NMB zimeingia katika ushirikiano utakao wawezesha mamilioni ya watanzania kunufaika na huduma za kifedha nchi nzima.
Hatua
hii itawawezesha watanzania wengi zaidi kufikiwa na huduma za kifedha
kwa njia ya mtandao ikiwa ni sehemu ya kufanikisha azma ya serikali
ambayo inazitaka taasisi mbalimbali za kifedha kuwafikia wananchi na
huduma zao hasa kwa maeneo ya vijijini.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi huo, Naibu Mkurugenzi wa Kampuni ya Halotel, Le Van
Dai amesema kuwa ni hatua nyingine kubwa katika utoaji wa huduma za
kifedha kupitia simu za mkononi ambapo sasa huduma ya Halopesa itakuwa
imeunganishwa na benki ya NMB ili kuwawezesha wateja kufanya miamala kwa
urahisi zaidi.
Dai
ameendelea kuwa ushirikiano huo, umeunganisha taasisi kubwa zenye
wateja wengi na zilizosambaa kwa kiasi kikubwa nchini. Tunatarajia
huduma hii itapunguza kadhia kwa watumishi wa taasisi za umma, wakiwemo
walimu na watu wa sekta zingine wakiwemo wakulima, wavuvi na wafanya
biashara wanaoishi vijijini ambako huduma za kibenki hazijafika kote.
Maeneo haya kwa kiasi kikubwa hutegemea njia ya simu za mkononi kuweza
kutoa fedha au kuweka kwa njia ya haraka na usalama zaidi.
“Ushirikiano
huu ni wa kipekee katika kurahisisha maisha ya watanzania ambao
wamekuwa wakipata tabu kupata huduma za kifedha kutokana na maeneo
wanayoishi. Sisi kama Halotel hadi sasa tumewafikia watanzania kwa zaidi
ya asilimia 95. Hivyo ni dhahiri kwamba wateja watakaojiunga nasi
wataweza kutoa au kuweka fedha huko huko waliko kupitia kwa mawakala
wetu ambao wameenea nchi nzima,” aliongezea Dai.
“Tunatambua
changamoto ambazo kwa kiasi kikubwa zimekuwa zikiwasibu Watanzania hasa
wa kipato cha chini. Kwani wengi wao walikuwa wanakwama kuweza kupata
huduma za kifedha kutokana na miundombinu kutowafikia. Mpaka hivi sasa
Halotel ina mawakala zaidi ya 30,000 walioenea nchi nzima. Hii
itawawezesha wakazi wa maeneo ambayo hayakuwahi kuwa na mawasiliano
kabisa au huduma za kibenki sasa kuweza kupata huduma za kifedha kupitia
simu zao za mkononi,” alimalizia Naibu Mkurugenzi wa kampuni hiyo.
Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Huduma Binafsi za Kibenki wa NMB,
Boma Raballa, amesema ushirikiano huo ni mafanikio mengine makubwa ya
kibiashara kwao hususani katika kupanua wigo wa huduma zake na namna
itakavyoweza kuunganisha teknolojia ili kuwarahisishia watanzania kupata
huduma za kifedha popote walipo.
“Benki
ya NMB ni ya kwanza kutoa huduma za kipekee na zenye ubunifu wa hali ya
juu na tunaamini ushirikiano huu utatuwezesha kuwafikia watanzania
wengi zaidi. Watanzania wanahitaji huduma za kifedha muda wowote na
mahali popote walipo. Hivyo kuja kwa ushirikiano huu kutawaletea uhakika
wa kupata fedha tena kwa njia rahisi kabisa kwa kutumia simu zao za
mkononi maana sio muda wote watakuwa karibu na mashine zetu za kutolea
fedha (ATM) au matawi ya benki yetu,” alisema Raballa
“Kwa
kushirikiana na Halotel tunaamini tutakuwa tumefanikisha lengo la
serikali na benki yetu kwa ujumla katika kuwafikia watanzania wengi
zaidi. Hii inamaanisha kuwa wateja wa kampuni hizi mbili ambazo
hawajafikia na huduma aidha za NMB au Halotel basi watafikiwa kwa
pamoja. Mbali na kurahisisha huduma lakini pia itasaidia kwa kiasi
kikubwa kurahisisha kuboresha na kurahisisha hali ya maisha na uchumi
kwa watanzania, yaani kwa watoa na wapokea huduma,” aliongezea Raballa.
0 maoni :
Chapisha Maoni