Zilizopendwa Zaidi

Wapendwa
Breaking
Inapakia...

DUA MAALUM ALIYOIFANYA SHEIKH MKUU WA DAR ES SALAAM KWENYE MSIBA WA ALIYEKUWA MWENYEKITI WA FREEMASON E.A TANZANIA ANDY CHANDE YAZUA TAFRAN


Kufuatia Sheikh Mkuu wa Dar es salaam, kusoma dua maalum ya kumwombea marehemu Andy Chande aliyekuwa na imani kinzani,[​IMG]
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Musa Salumu mwishoni mwa wiki iliyopita alizua utata katika kona mbalimbali za kijamii kufuatia kufanya dua maalumu ya kumwombea aliyekuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Freemason Afrika Mashariki, marehemu Sir Jayantilal Keshavji ‘Andy Chande’ (pichani).

Tukio hilo lilifanyika Aprili 21, mwaka huu katika Shule ya Sekondari ya Shabani Robert na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa nchi, akiwemo Rais Msaatafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin William Mkapa sanjari na wanafunzi wengine waliowahi kusoma katika shule hiyo.

[​IMG]
Sir Andy Chande alifariki dunia, Aprili 7, mwaka huu nchini Kenya kwa maradhi ya presha na kuzikwa katika Makaburi ya Baniani, Makumbusho jijini hapa kwa kuchomwa moto.

Katika enzi za uhai wake, Sir Andy Chande aliwahi kuweka wazi kuwa yeye ni mfuasi na kuhani mkuu wa Jumuiya ya Freemason, jumuiya ambayo inaaminika na baadhi ya watu kwamba iko kinyume na mafundisho ya dini za Kiislamu na Kikristo. Katika tukio hilo la kuwakumbuka waasisi wa shule hiyo, Shehe Alhadi aliongoza dua maalumu kwa upande wa dini ya Kiislamu kwa ajili ya kumwombea marehemu Chande jambo lililoibua mjadala mkubwa.

MSIKIE HUYU

Baadhi ya watu walihoji kuwepo kwa shehe mkuu wa Dar kwenye dua hiyo wakati marehemu alijulikana kuwa ni Freemason ambayo wengi hawaiamini kama ina sera za Mungu. Msikie huyu:

“Mimi binafsi sidhani kama ni sahihi kumfanyia dua mtu ambaye aliwahi kuweka wazi kwamba yeye yupo upande wa kushoto, tena akiwa mwenyekiti na kuhani mkuu wa jumuiya ambayo inaaminika inakwenda kinyume na maadili ya Kimungu,” alisema Kimashi John katika ukurasa wake wa Facebook.

Mbali na mtu huyo, mijadala mingi siku hiyo ilikuwa kuhudhuria kwa shehe mkuu kwenye shughuli hiyo.

Gazeti la Uwazi, baada ya kuyasikia hayo, liliamua kumtafuta Shehe Alhadi mwenyewe ili kutoa ufafanuzi juu ya suala hilo.
Akizungumza na mwandishi wetu kwa njia ya simu, Shehe Alhadi alikuwa na haya ya kusema:

“Katika dua niliyoiomba siku ile hakuna neno nililosema kwamba Mungu aiweke roho ya marehemu Chande mahali pema peponi. Unaweza kusikiliza tena rekodi za ile dua, nilichokifanya ni kumwombea kwa Mwenyezi Mungu amlipe kwa mambo yote aliyoyafanya duniani maana yeye ndiye hakimu wa mwisho.”

Aidha, katika hatua nyingine Uwazi lilipotaka kujua kama alishawahi kumpa elimu ya dini ya Kiislamu, marehemu Sir Chande ikiwa ni pamoja na kumtaka asilimu, Shehe Alhadi hakuwa tayari kulizungumzia hilo zaidi ya kukiri kwamba amekuwa akifahamiana na marehemu kwa muda
mrefu.
 
Source: Jamii Forum
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 maoni :

Chapisha Maoni