Zilizopendwa Zaidi

Wapendwa
Breaking
Inapakia...

TUNDU LISSU: MATUMIZI YA HOVYO YA MAMLAKA YA KIPOLISI LAZIMA YAKOME


Image result for tundu lissu images


Waheshimiwa salaam,

Nimetoka Polisi Bandari muda huu. Nilikwenda kumwona mtu aitwaye Ramadhani Mussa Hamisi alias Ukwaju ambaye yuko mahabusu ya Polisi Bandari tangu tarehe 4 ya mwezi huu.

Ukwaju anatuhumiwa kuhusika na mzigo wa magari ya kifahari yaliyokamatwa na Bwana Mkubwa Rais siku chache zilizopita.

Leo ni siku ya 23 yuko mahabusu. Hajapelekwa kwenye mahakama yoyote na hajashtakiwa kwa kosa lolote lile.

Suala lake limeshafika kwa DPP na kwa RPC Sirro tangu siku kadhaa zilizopita lakini kila mkubwa anayehusika anaogopa kutoa maamuzi ya kumpeleka mahakamani au hata kumwachia kwa dhamana ya polisi.

Haya ndiyo madhara ya Rais wetu kuingilia majukumu ya kisheria yasiyomhusu. Rais wetu anaweza kuwa Amiri Jeshi Mkuu lakini yeye sio askari polisi mwenye jukumu la kukamata wahalifu au kupeleleza makosa wanayotuhumiwa nayo.

Ijapokuwa ni Rais ndiye anayemteua DPP, yeye sio DPP na hana mamlaka ya kuamua nani apelekwe mahakamani na nani asipelekwe.

Sasa inapotokea Rais anakwenda kwenye matukio ya uhalifu, kama ilivyokuwa kwenye suala la Ukwaju, anawafanya watendaji wanaohusika nayo washindwe kufanya kazi zao kwa mujibu wa sheria.

Katika mazingira ya sasa ya 'utumbuaji majipu', watumishi wa umma wanaogopa kufanya maamuzi kwa hofu ya kutumbuliwa majipu, hasa kwa masuala ambayo yameshafikishwa kwa Rais kwa njia extra-legal kama hili la Ukwaju.

Matokeo yake haki za wananchi za kuwa huru zinakiukwa bila sababu za msingi.

Haya ni masuala ambayo TLS chini ya uongozi wangu inatakiwa kuyashughulikia. Hii ni sehemu ya agenda tutakayompelekea Rais na IGP na AG pamoja na Waziri mpya Prof. Kabudi tutakapoenda kuonana nao kama tulivyokwishawaomba.

Kila mmoja wetu, mawakili na wasiokuwa mawakili tuyapigie kelele matumizi mabaya ya mamlaka ya kiupelelezi na ya kipolisi yanayopelekea haki za wananchi wetu kuvunjwa namna hii.

Kelele zitasaidia, ukimya ni sawa na kuyaunga mkono matendo haya mabaya.

Wasalaam.

Tundu Lissu.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 maoni :

Chapisha Maoni