FIFA yaidhinisha kuwepo timu 48 kombe la dunia
Chama cha soka duniani FIFA
kimepanga kuwepo kwa michezo sita ili zipatikane timu zitakazoingia
katika fainali za kombe la dunia mwaka 2020.
FIFA imefafanua ni kwa namna gani timu 48 zitaweza kushiriki michuano hiyo.Rais wa shirikisho la soka Ulaya Aleksander Ceferin amesema kuwa amefurahishwa na hatua hiyo na nchi za Ulaya zitawakilishwa vyema.
Mchakato huo utakuwaje?
Kila mwanachama wa FIFA atakuwa na uwezo wa kuongeza walau timu moja katika michuano ya mwaka 2026.Mwenyeji wa fainali hizi ataingia moja kwa moja kama ilivyokua awali.
Mapendekezo hayo yapo hivi
Afrika - 9 kutoka timu za awali 5Asia - 8 kutoka timu 4 za awali
Ulaya - 16 kutoka timu 13 za awali
Marekani ya Kaskazini, Kati na Caribbean - 6 kutoka timu 4 za awali
Bara la Oceania - 1 kutoka timu 1 ya awali
Amerika ya Kaskazini - 6 kutoka timu 4 za awali
0 maoni :
Chapisha Maoni