Zilizopendwa Zaidi

Wapendwa
Breaking
Inapakia...

NAPE NA WAANDISHI WA HABARI


Heshima Kwenu wakuu,

Leo nmeamua kuwaletea update kutoka kwenye mkutano wa aliyekuwa Waziri wa Michezo wa awamu ya tano Nape Nnauye.

Karibuni.

=======

UPDATES;


=======

13:08hrs: Nipo hapa Protea hotel, Mheshimiwa Nape bado hajafika. Ntamsubiri hapa hapa.

Ametokea mtu anayeitwa Iddi Suleiman ambae ni meneja wa Protea na kudai mkutano hautakuwepo na waandishi walipombana nani kazuia, alisema akaulizwe RPC wa Kinondoni.
Nape anaongea na waandishi wa habari nje yanHoteli akiwa juu ya gari

Nape: Wapuuzi, nimekuja hapa wananitolea bastola eti rudi kwenye gari, nimepigana kuiweka CCM madarakani anakuja mpuuzi eti usishuke kwenye gari, mimi nape sina kinyongo na uamzi wa rais wangu, kama sikumshawishikunichagua hivyo hata kuniacha ni sawa.

Nimejitahidikutimiza wajibu wangu, tusihangaike na Nape tuhangaike na Tanzania inapokwenda nimekuwa mzalendo na muungwana, nimekuwa ninatimiza wajibu wangu
Mimi ndo nlisimama kuiinua CCM, nitasemakweli daima na fitina kwangu mwiko, kinachotukutanisha sio magwanda ya kijani, ni imani, nimefundisha na mzee Nnauye kusema kweli na kusimamia ninachokiamini, mimi nlishawahikufukuzwa CCM

Usipopita kwenye matatizoya kisiasa hutakomaa, Ili mbegu iote shuti ioze, nimepandambegu ya kupigania haki, Tanzania ni yetu nchini yetu. Mwalimu, Kawawa waliondoka na sisi tutaondoka.
Lengo la kuja hapa ni kumshukuru rais kwa alichokifanya, namshukuru kwa kuniamini kwa mwaka mmoja, nampongeza Mwakyembe naye ni mwanahabari.
Nimefurahi kufanya kazi na nyie, muungeni mkono Mwakyembe na Rais Magufuli
Tudumishe amani na upendo wa nchi yetu, Nape ni mdogo kuliko nchi, wakati wa aliyeniteua ameniondoa mimi nitaendelea kuwatumikia

Polisi wamezuia gari ya Nape isiondoke, ameshuka kwenye gari anamsikiliza kamanda wa polisi Kinondoni
Nape anawataka waandishi wa habari waondoke, anadai hakuna la kuwaambia tena

WhatsApp Image 2017-03-23 at 2.23.08 PM.jpeg

View attachment 485512
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 maoni :

Chapisha Maoni