Zilizopendwa Zaidi

Wapendwa
Breaking
Inapakia...

MAKONTENA YALIYOKAMTWA:NIPO TAYARI IKIBIDI HATA KUNYONGWA


 Naomba ni declare interest kuwa, mimi ni mmoja wa wataalam wanaouhusika na ishu iyo ya mchanga.

 
17309816_10208672062578182_5022295759993761281_n.jpg
Mh rais, nikiwa na akili timamu, naomba leo niseme, iwapo itathibitika kuwa Accacia wanaiibia serikali kwa kuweka kiasi kikubwa cha dhahabu kwenye makontena, naomba uamuru maafisa wako wa intelijensia waende ofisi za JF wachukue details zangu, ili niweze kukamatwa na ninyongwe hadharani.
Pia nawaomba mod, muweke details zangu hadharani ili nifahamike, na iwapo mnataka details nyingine, mni-pm ili niwewe kuwapa na hata ikibidi picha.

Kifupi naomba nieleze kile ambacho kipo kwenye makontena.
Kilichopo kwenye makontena kwa asilimia kubwa ni copper(Cu) , ifufuatiwa na silver (Ag) na dhahabu (Au) haizidi asilimia 0.05.
Yule asifa wa bandari aliyesema kuwa zaidi ya asilimia 90 ni dhahabu ni muongo na anapaswa kuiomba radhi Acacia na watanzania kwa ujumla na atumbuliwe kwenye nafasi yake.

Kiwango kilichopo kwenye yale makontena zaidi ya 256 ni kati ya sililimia 0.012 -0.02, g/t
Iwapo yatazidi asilimia 0.05g/t, narudia NAOMBWA NINYONGWE HADHARANI, kwani nami nimehusika kwa namna moja au nyingine kuiibia serikali.

Mh spika alidhani kiwango cha asilimia 0.02 kuwa ni kidogo na hauwezi kupata faida iwapo utalisafirisha kontena kutoka mgodini mpaka china japani au Ujerumani.
Naomba nimuulize, anajua gharama ya kusafirisha hilo kontena? kifupi haizidi milioni 8.

Nikija kwenye mchanganua wa hiyo asilimia 0.02 kwa contena, naomba nimfafanulie mh spika kama ifuatavyo:-

(1) 0.02% hii ni gram kwa tani, kwa maana hiyo hii ukiizidisha kwa tannage zilizopo (eg 20.5tn), utapata 0.41%.
(2) Hii 0.41 ili upate ppm, unatakiwa uizidishwa kwa 10000, utapata 4100ppm au g/t.
kwa maana nyingine, yule mtaalam wa TMAA aliwaambia kwenye kila container kuna takriban kilo 4.1. sasa hii ni ndogo?
(3) Kwa sasa kilo ya dhahabu ni takribani mil 90. 90x4=36m.
sasa iwapo utasafirsha container moja kwa 10m, huoni kuna faida?

Pia kamati ya bunge kupitia spika alidai kwa mwaka AcaciaBuzwagi na Bulyanhulu huzalisha takribani idadi ya makontena elfu 50, na kwa maana hiyo contena milioni moja yameisha safirishwa. HUU sio UKWELI.
Ukweli ni kwamba hizo ni tani za mchanga wa dhahabu na sio idadi ya contena.

Mpaka sasa, migodi ya Bulyanhulu na Buzwagi wameisha safirisha makontena yasiozidi elfu 50.

Mpaka sasa Bulyanhulu peke yake wamesafirisha contena sizizozidi elfu 42. Sasa izo contena 1m, zimetoka wapi?
Mh rais kuna wanakupotosha, na hili utalithibitisha kupitia sample zilizochukuliwa na mh waziri mkuu jana katika mgodi wa Buzwagi, kwani kati ya makontena aliyochukua sample, moja wapo ni kotena ambalo lililkua na seal na document zote za serikali na lilikua tayari kusafirishwa kwenda ujerumani.
Baada ya tamko la rais kontena hilo lilirudishwa mgodini pamoja na makontena mengine 3, yakiwa tayari yamefika Isaka.

My take:-
Kwenye hili sakata la mchanga, mihemuko isitumike, wawekezaji wa Acacia hawamuibii mtu, kwani hata kama kungekua na 90% ya dhahabu, TMAA huchukua sample pia, kiasi kwamba wangeweza kuiambia serikali kuwa, Acacia wanawaibia kwa kutoa takwimu za uongo.
Iwapo mikataba haiwafaidishi watanzania, ifanyiwe review, kwani Acacia hutumia mikataba hiyo hiyo kufanya calculation zao.
Iwapo itathibitika kuwa acacia pia hawawaibii watanzania kwa kuficha dhahabu kwenye mchanga, basi pia katibu mkuu aombwe radhi.

Tafadhali mod naomba msiifute hii thredi kwani nachokiongea nakiamini na nakifanyia kazi.
Source: Jamii Forum

 
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 maoni :

Chapisha Maoni