Zilizopendwa Zaidi

Wapendwa
Breaking
Inapakia...

MAHAKAMA KUU YAMWACHIA HURU MBUNGE PETER LIJUAKALI

 Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imetengua Hukumu iliyotolewa na Mahakama ya wilaya Kilombero dhidi ya Mbunge Peter Lijualikali hivyo katika kesi ya msingi Lijualikali amekutwa hana Hatia.


Mbunge Lijualikali alihukumiwa kwenda Jela Miezi Sita(6) bila faini na Mahakama ya Kilombero. Alikuwa akikabiliwa na Kesi ya kufanya vurugu wakati wa Uchaguzi 2015.



IMG_20170330_113841.jpg

Mahakama Kuu kanda ya Dar ES Salaam imetengua hukumu iliyotolewa na Mahakama ya Wilaya Kilombero dhidi ya Mbunge Peter Lijualikali baada ya kukubaliana na warufani kwamba hati ya mashtaka iliyomtia hatiani ilikuwa na upungufu.
Uamuzi huo umetolewa leo mbele ya Jaji Ama- Isaria Munisi baada ya kupitia sababu za kupinga mbunge huyo kutiwa hatiani na kuhukumiwa kifungo cha miezi sita jela.

Peter aliwakilishwa mahakamani na Wakili Tundu Lissu na Fred Kiwelo wakati Jamhuri ilikuwa ikiwakikishwa na Wakili wa Serikali, Faraja Nchimbi.

Mshtakiwa mwingine aliyehukumiwa kifungo cha nje, Stephani Mgatta adhabu yake pia imetenguliwa.

Rejea;

=> Tundu Lissu amesema kuwa CHADEMA itakata rufaa dhidi ya hukumu ya Mbunge kwenda jela miezi sita

=> Mbunge wa Kilombero(CHADEMA) Mh. Lijualikali, afungwa jela miezi sita

 
Source: Jamii Forum
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 maoni :

Chapisha Maoni