Chumba cha kaburi alimozikwa Yesu chafunguliwa tena Israel,
Chumba cha kaburi alimozikwa Yesu chafunguliwa tena Israel
Chumba
kidogo kinachofunika kaburi ambako inaaminika Yesu Kristo alizikwa
kimefunguliwa rasmi tena baada ya kufanyiwa ukarabati kwa miezi tisa.
Chumba
hicho ambacho kinapatikana katika Kanisa la Kaburi la Yesu Kristo
katika maeneo ya mji wa zamani wa Jerusalem kilikuwa kimekuwa dhaifu
sana kiufundi.Aidha, kilikuwa limebadilika rangi na kuwa karibu rangi nyeusi kutokana na masizi ya mishumaa mingi ambayo huwashwa eneo hilo.
Mzozo kati ya madhehebu matatu ambayo kwa pamoja husimamia kanisa hilo - Kanisa la Kiothodoksi la Ugiriki, Kanisa la Kiarmenia na Kanisa Katoliki la Kirumi - ulichelewesha ukarabati huo kwa miongo mingi.
Antonia Moropoulou, aliyesimamia ukarabati, amesema chumba hicho sasa kimepata tena rangi yake asili inayokaribia hudhurungi.
Chumba hicho kilifanyiwa ukarabati mara ya mwisho mwaka 1810.
0 maoni :
Chapisha Maoni