Brazil yafuzu Kombe la Dunia 2018 baada ya kulaza Paraguay
Brazil imekuwa taifa la kwanza kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia ambazo zitachezewa nchini Urusi mwaka ujao.
Walifuzu baada ya kulaza Paraguay 3-0, nao Argentina na Uruguay wakashindwa.Hii ina maana kwamba sasa Brazil hawaweza kumaliza chini ya nafasi nne miongoni mwa mataifa ya Amerika Kusini, ambapo mataifa ya kwanza manne ndiyo hufuzu.
Brazil waliwashinda Paraguay kupitia mabao ya mshambuliaji wa Liverpool Philippe Coutinho, nyota wa Barcelona Neymar na mchezaji wa Real Madrid Marcelo.
Neymar pia alipoteza mkwaju wa penalti.
Brazil kwa sasa wamo alama tisa mbele ya Colombia ambao wanashikilia nafasi ya pili.
Huo ulikuwa ushindi wa nane kwa Brazil chini ya Tite.
Paraguay, wamo alama chini ya nne bora, zikiwa zimesalia mechi nne kuchezwa.
Argentina wanakabiliwa na kibarua kufuzu baada ya kushindwa 2-0 na Bolivia na kushuka hadi nambari tano, alama moja nyuma ya Chile.
Uruguay, waliochapwa 2-1 na Peru mjini Lima Jumanne, wamo nambari tatu.
Taifa litakalomaliza nafasi ya tano litacheza mechi mbili za muondoano (nyumbani na ugenini) dhidi ya taifa kutoka Oceania.
Source: Swahill BBC
0 maoni :
Chapisha Maoni