Sherehe
ya kula nyama ya mbwa iliogubikwa na utata katika mji wa Yullin nchini
China imeanza licha ya ripoti za awali kwamba ilikuwa imepigwa marufuku
mwaka huu.
Sherehe hiyo hufanyika kila mwaka katika mkoa wa Guangxi.
Mapema mwaka huu ,wanaharakati walidai kwamba wafanyibiashara waliagizwa na mamlaka kutouza nyama ya mbwa.
Lakini wamiliki wa vibanda vinavyouza nyama hiyo waliambia BBC hawajasikia lolote kuhusu hatua hiyo kutoka kwa maafisa.
Mnamo tarehe 15 mwezi Mei, maafisa wa mji walithibitisha kwamba hakuna marufuku yoyote.
Siku
ya Jumatano, ripoti kutoka Yullin zilisema kuwa mbwa waliokufa
walionekana wakiwa wametundikwa katika ndoano za nyama katika vibanda
ndani ya soko la Dongkou ambalo ndio kubwa mjini humo.
Mwanaharakati
mmoja aliambia BBC kwamba alikatazwa na maafisa wa polisi kuingia
katika soko la Dashichang ambapo inaaminika mbwa walikuwa wanauzwa.
Katika
sherehe za miaka ya nyuma kumekuwa na mzozo kati ya wauzaji nyama ya
mbwa na wanaharakati waliojaribu kuwaokoa mbwa waliopangwa kuchinjwa.
0 maoni :
Chapisha Maoni