Zilizopendwa Zaidi

Wapendwa
Breaking
Inapakia...

WADAU WA HABARI NA HAKI ZA BINADAMU WALAANI KITENDO CHA MAKONDA KUVAMIA KITUO



WADAU wa habari, mashirika ya haki za binadamu na asasi za kiraia zinazojihusisha na utawala wa kidemokrasia katika nchi mbalimbali duniani, zimetoa kauli ya kulaani vitendo vya ukandamizaji wa uhuru wa habari,.

Tamko lao linakuja kufuatia kikao cha siku mbili kilichoketi juzi na jana mjini Kampala, Uganda ambapo pamoja na mambo mengine walijadili hali ya uhuru wa kujieleza na upatikanaji wa taarifa katika nchi mbalimbali.

Katika tamko lao lililosainiwa na jumla ya mashirika, taasisi na asasi za kiraia 33 wamesema.

“Tunalaani kwa nguvu zote uvamizi haramu uliofanywa na Mkuu wa Mkoa ili kulazimisha kurushwa kwa kipindi ambao ndiyo umesababisha Waziri wa Habari kufukuzwa baada ya kuingilia na kuunda tume ya uchunguzi dhidi ya suala hilo.”

Itakumbukwa kuwa tarehe 17 Machi, mwaka huu saa nne na dakika 40 usiku, Paul Makonda (Daudi Albert Bashite) aliongoza uvamizi katika kituo cha utangazaji cha Clouds Media akiwa na askari sita wenye silaha, kilazimisha kurushwa kwa video inayohusu mwanamke anayedaiwa kuzaa na Askofu Josephat Gwajima.

Nape Nnauye, waziri wa habari alilaani tukio hilo baada ya kukitembelea kituo hicho na kuunda tume ya uchunguzi iliyoongozwa na Dk. Hassan Abbasi, Msemaji Mkuu wa Serikali. Hata hivyo Nape alifukuzwa kazi siku moja baada ya tume hiyo kukabidhi kwake ripoti iliyomtia hatiani Makonda.

“Vitendo vya mkuu wa mkoa, na kufukuzwa kwa waziri aliyepinga uvamizi katika kituo cha Clouds Media ni kinyume na sheria na Katiba ya Tanzania.

“Inakadiriwa zaidi ya matukio 10 ya ukamataji na unyanyasaji wa wanahabari yameripotiwa kufanywa na na wakuu wa wilaya kwa kipindi kisichozidi miaka miwili,” imesema taarifa hiyo.

Miongoni mwa mashirika yaliyotoa tamko hilo la pamoja ni Shirikisho la kimataifa la wanahabari la Ubelgiji, taasisi ya vyombo vya habari vya Ghana, Chama cha waandishi wa habari wa Rwanda, chama cha waandishi wa habari wa Cameroon na kituo cha mafunzo ya vyombo vya habari Liberia.

Mengine ni Chama cha wanahabari wa Guinea, chama cha taifa cha wanahabari wa Tunisia, taasisi ya maendeleo ya sekta binafsi na za umma ya Nigeria, Mtandao wa Taifa wa Taasisi za Haki za Binadamu Kenya, taasisi ya haki ya kujua (right to know) ya Afrika Kusini.

Source : Jamii Forum
 

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 maoni :

Chapisha Maoni