Hiyo inatokana na mwenyekiti wa CCM wilayani Chamwino, Charles Ulanga kuhoji sababu za kutajwa katika orodha ya walioghushi vyeti vya kidato cha nne wakati hajawahi kusoma elimu ya Sekondari

Utata huo umeibuka mkoani Kigoma, ambako jina la mganga mkuu wa mkoa limetajwa, likionekana kutumiwa na mfanyakazi wa Hifadhi ya Gombe iliyoko Kigoma
Akizungumza na gazeti hili jana baada ya jina lake kuwa miongoni mwa wenye vyeti feki, Ulanga, ambaye pia ni Mratibu wa Elimu wa Kata ya Buigiri wilayani Chamwino mkoani Dodoma, alisema wakati wa uhakiki alipeleka cheti cha darasa la saba na cha ualimu daraja la tatu 'A'.
"Nawashangaa wapi walipopata cheti cha kidato cha nne kwa sababu mimi nilipeleka vyeti viwili; cha darasa la saba na cha ualimu. Sasa hiki cha kidato cha nne walichokikuta feki sijui wamekitoa wapi?" alihoji Ulanga
Mwenyekiti huyo alisema baada ya kumaliza darasa la saba aliomba kujinga na masomo ya ualimu kama utaratibu ulivyokuwa ukitaka wakati huo
Alijiunga na Chuo cha Ualimu Bustani kilichopo wilayani Kondoa mwaka 1980 na kutunukiwa cheti daraja la tatu "B"
"Wakati ule ulikuwa unaomba kwenda darasa saba niliomba kwenda chuo cha ualimu nikakubaliwa nikaenda Bustani na nilipata cheti cha ualimu daraja la tatu "B", alisema Ulanga
Chanzo: Mwananchi
0 maoni :
Chapisha Maoni